Tuesday, November 24, 2009

Miwani ya jua unayoivaa ni salama kwa macho yako?


Wengi wanapendelea kuvaa miwani bila ya kupata ushauri wa daktari huku wengine wanaamua kuvaa miwani bila kuwa na tatizo lolote kwenye macho yao ili mradi wanaona miwani inawapendeza. Miwani mingi ya macho inatumika bila kuwaona wataalam wa macho hiyo ni hatari kubwa sana kwako.
Leo tunazungumzia kuhusu miwani ya jua. Wengi wanapenda kununua miwani hii mitaani na kuijaribu na kama wanaipenda wanaamua kuivaa.
Kuwe na mvua au jua watu wengi hupendelea kuficha nyuso zao kwa miwani kwa jinsi wanavyotaka.
Unaweza kuwa na miwani yenye fremu nzuri na kioo cha kutia nakshi lakini je uko kwenye vipimo vya macho?
Yaani miwani yako hiyo inakidhi kweli mazingira ya kukukuhami na jua? Vipi shauri wa miwani inayoacha nafasi ya kuhangaika kuangalia juu au chini na wakati mwingine kioo hakifai kabisa, tazama pamoja na urembo huenda ukapata mikunjo ya ngozi na hili hutalipenda.
Kama unaweza pata ushauri wa daktari kama hujaamua kuwa na miwani kwa ajili ya usalama na ulinzi wa macho yako.

Pendezesha makalio yako kwa kufanya haya


Makalio yetu ndiyo yanayotoa shepu fulani kwa mwanamke katika vivazi na ukiyaachia ovyo yanaweza kukuletea mushkeli na kama ukiyatengeneza hata yale makalio yanayosifiwa sana.
Wanawake wengi kwa sasa wanapenda kurekebisha makalio yao ili kuyapatia ukubwa unaostahili kwa jinsi wao wanavyopenda.
Tatizo hili halipo hapa nchini lakini wapo walionitupia swali na sasa inabidi nikiri kuwa lipo sana Marekani na mpasuaji wa masuala ya urembo wa Miami Dk Constantino Mendieta amethibitisha.
Mtaalam huyu amezungumzia sana utunzaji wa makalio daraja la kwanza ndiyo yanayotakwa sana. Ni kama vile umeuchukua moyo halafu ukaugeuza chini juu,haya ndio dizaini ambayo Marekani wanalilia sana.
Watu wa huko wanajimwaga katika majumba ya upasuaji kupata shepu hiyo adimu, na anayewachengua sana.
Kama unataka kuwa na shepu bomba fuata hatua zifuatazo:
1. Fanya masaji na losheni zinazoimarisha na kutengeneza ngozi nyororo katika mapaja yako,ukianzia chini ya makalio mara mbili kwa siku.
2. Ondoa miinuko midogo midogo isiyotakiwa nyuma yako kwa kuskrabu mara mbili au tatu kwa wiki ukiwa na salt scrub.
3. Pamoja na matatizo ya michuchumio,ivae ili kukupata nafasi ya kutembea kwa miondoko ya twiga inayotoa nafasi nzuri kwa makalio kuwa na mvuto.
4. Tafuta namna nzuri ya kuficha michirizi ya kunyooka kwa misuli ya mwili.
5. Mazoezi yatakufanya uwe mtu tofauti zaidi, pandisha ngazi kwa dakika kumi au zaidi na kisha chukua mazoezi ya kubana makalio yako na sehemu ya kiuno kwa kusukuma kwa ndani na kutulia hivyo kwa sekunde tano na kujiachia na unaweza kufanya hivyo unavyotaka.
Pia unaweza kuongeza uzuri wa makalio yako kwa kuhakikisha kwamba unakula vyema na unakula lishe inayostahili.

Umakini watakiwa katika chaguo la viatu


Unapoamua kuvaa aina ya viatu unakuwa na sababu za aina mbalimbali. Wengi hupendezewa na uvaaji wa viatu virefu na wengine hupendelea kuvaa viatu visivyo na kisigino flat shoes.
Wengi wetu hasa wakinadada wamekuwa wakipenda zaidi kuvaa viatu virefu licha ya kujua kuwa wakati mwingine viatu hivyo huleta madhara katika afya zao. Mara nyingi viatu virefu vimekuwa vikivaliwa na watu ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa kutumia miguu na hivyo kuharibu afya za miguu yao.
Kwa upande mwingine flat shoes vimekuwa vikivaliwa sana na watu ambao wana uzito mkubwa na wale ambao hawapendi kuvaa viatu virefu.
Pia viatu hivi vimekuwa vikivaliwa kulingana na aina ya nguo uliyovaa kwani wakati mwingine nguo huendana na aina ya viatu kitu ambazo watu wengi huwa hawakizingatii mavazi mengine yanatakiwa kuvaliwa na flat shoes.
Na kitu kingine cha kuzingatia ili upendeze na aina hii ya viatu unatakiwa kuchagua vinavyoendana na rangi ya nguo uliyovaa.
Kuna aina nyingi ya viatu vya aina hii ambavyo vimekuwa vikiuzwa madukani lakini ni muhimu wakati unataka kununua kiatu cha aina hii unatakiwa kuzingatia malighafi ambayo imetengeneza kiatu.
Viatu vya ngozi huwa ni vizuri zaidi kwani huvaliwa muda mrefu bila kuharibika tofauti na viatu vya plastiki ambavyo hudumu kwa muda mfupi na kuchanika chanika.